Mrs. Agness Gabriel Sanga
InspireFikra PodcastMrs. Agness Gabriel Sanga
Je, wewe ni Mfanyabiashara, Mfanyakazi wa Taasisi ya Umma/binafsi au ni Mwanafunzi? Je, umekuwa ukihisi kuna kitu kinakosekana katika maisha yako na katika kazi unayofanya? Huenda huo ukawa wito wa mwaliko kutoka kwa Muumba wako, akikualika kujaribu mapenzi na kusudi lake katika maisha yako. Unajiuliza Sasa ufanyaje? Naam, ndiyo sababu tuko hapa. Kazi yetu ni kuhamasisha Mabadiliko ya mtu binafsi kwa kufanywa upya Akili na Mtindo wa Maisha kupitia mafundisho ya neno. Ili, uweze kuwa Wakili Mwema, Mwenye Hekima na Mwaminifu kupitia Kazi/nafasi uliyonayo kwaajili ya Ufalme wa Mungu.