Kwa miaka kadhaa nchini Tanzania kumekua kukidaiwa kipengele katika katiba kitakacho ruhusu mgombea huru asiye na chama. Wapo waliothubutu kwenda mahakamani wakashinda na hakuna mabadiliko yaliyotokea. Shida iko wapi, na ni nini kinaogopwa kuwa na mgombea huru? Je kwa wakati huu kuna uhitaji wa kuwa na mgombea huru asiyefungamana na chama chochote cha siasa? Karibu kusikiliza wataalam wa siasa na wataalam wa asasi za kisheria wanasemaje kuhusu hili